WASHIRIKA WAWEZESHAJI

WASHIRIKA WAWEZESHAJI

Peak inaendeleza mradi wa Ngualla kwa kushirikiana na taasisi ya  wawekezaji wa muda mrefu ya  Appian Natural Resources (‘Appian’) na Shirika la fedha la kimataifa (‘IFC’). Pamoja na kutoa fedha ya uwekezaji, Appian na IFC wameweza kuvutia uzoefu mwingi na wa kina na mitandao katika maeneo ya metali na madini, fedha kimataifa na rasilimali kwa maendeleo ya mradi. Appian na IFC kwa pamoja wamewekeza katika uwiano wa 80:20.

APPIAN MSHAURI WA MITAJI

Mfuko wa Appian Natural Resources ni mfuko wa uwekezaji wa muda mrefu katika uwezeshaji mitaji, ambao umeanzishwa mahsusi kuwekeza katika sekta ya metali na madini . Appian ina njia ya kipekee ya uwekezeji kwa njia ya kushirikiana ambapo hutafuta kushirikiana na wamiliki wenyeji, mameneja na wawekezaji ili kuhamasisha utaalamu wake wa kimataifa wa uendeshaji na fedha. Timu hii yenye uzoefu ni nyongeza kwa Peak ikiwa imeshajenga na kusimamia Zaidi ya migodi 60 inyofanya kazi mpaka sasa (30 ndani ya Afrika) na ikifanyia kazi Zaidi ya dola za marekani bilioni 200 kwa miamala ya shughuli za maendeleo ya madini.

Website 网站 Website
IFC

IFC, mwanachama wa Benki ya dunia, ni taasisi kubwa ya maendeleo ya kimataifa inayolenga kwenye sekta binafsi tu. Ikifanya kazi na makampuni binafsi katika takribani nchi 100, IFC hutumia mtaji, utaalamu na ushawishi wao kusaidia kuondoa umaskini uliokithiri na kuongeza ustawi wa ubia. Katika Mwaka wa fedha wa 14, IFC ilitoa zaidi ya dola za Kimarekani billioni 22, katika kugharamia kuboresha maisha katika nchi zinazoendelea na kukabiliana na changamoto muhimu za maendeleo. Mpaka sasa IFC imewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 400 nchini Tanzania. IFC huleta nguvu katika mahusiano ya serikali ya nchi na viwango vya juu vya utunzaji wa mazingira ya.

Website 网站 Website