WAKURUGENZ

John Jetter

Mkurugenzi asiye mwendeshaji
Shahada ya Sheria na Uchumi

John ana uzoefu wa kina katika masuala fedha ya kimataifa na uzoefu wa M &A  amewahi kushikilia nyadhifa mabalimbali kama  Mkurugenzi Mtendaji, mkurugenzi na Mkuu wa Benki ya uwekezaji ya JP Morgan Ujerumani na Austria, na mjumbe  wa baraza la Ulaya  la ushauri la JP Morgan huko London. Ana uelewa mkubwa wa tasnia ya Rare Earth, amekuwa anashiriki kikamilifu katika mazungumzo na utekelezaji wa  makubaliano ya uanzishwaji wa baishara ya Rare Earth

Jonathan Murray

Mkurugenzi asiye Mtendaji
Shahada ya Sheria na Biashara

Jonathan ni mshirika katika kampuni inayojitemea ya sheria ya makampuni makubwa inayoitwa  Steinepreis Paganin, iliyopo Perth, Magharibi wa Australia. Amabobea katika upatikanaji wa mitaji ya ndani ya makampuni, aina zote za ununuzi na uuzaji wa makampuni, utawala na usimamizi wa kampuni. Sasa yeye ni Mkurugenzi asiye Mtendaji wa Hannans Reward NL, Laguna Resources NL na Kalgoorlie Mining Company Limited.

Peter Meurer

Mwenyekiti asiye Mtendaji
Shahada ya uzamivu kutoka RMIT

Peter anao uzoefu wa kazi wa kipekee na unaojulikana kwa zaidi ya miaka 40 katika sekta ya kifedha katika mashirika na kwa sasa ni Mwenyekiti asiye mtendaji wa Nomura Australia. Alijiunga na Namura kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2009 na kabla ya hapo alishika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Citigroup naMerrill Lynch. Peter ana mkakati imara na amejijengea uhusiano wa kuaminika wa ushauri kupitia miamala mingi inayohusiana na masuala ya masoko ambapo alihusika katika masuala yote yahusuyo fedha katika mashirika ikiwa ni pamoja na kuinua mitaji, kupata mikopo ushauri wa mashirika ikiwa ni pamoja na uongozi na utawala.

Tony Pearson

Mkurugenzi asiye mwendeshaji
Shahada ya kwanza ya Biashara, Uhasibu na Fedha

Tony ni mkurugenzi mzoefu katika uendeshaji wa rasilimali katika viwango vya kimataifa. Kwa sasa ni Kamishna katika Tume huru ya Mipango, kabla ya hapo alikuwa Mtendaji wa TSX/HKEx iliyosajiliwa katika soko la hisa yenye makao yake huko Hong Kong, ambako alikuwa na jukumu la uanzishwaji wa mikakati ya kampuni. Tonny pia ana uzoefu wa miaka 15 wa biashara, uwekezaji wa kibenki katika tania ya rasilimali asilia katika Pwani ya Asia, hivi karibni kama Mkurugeni Mtendaji HSBC