TIMU YA UONGOZI

Peak Resources ni mwendelezaji  pekee wa Rare Earth aliye na vyote yaani wataalamu waandamizi wa uzalishaji wa Rare Earth na utaalamu wa mauzo. Kampuni imeakisi ujuzi huu katika muundo wa uhandisi na Upembuzi Yakinifu wa Kimtaji. Pamoja na uzoefu wa uendeshaji , utaalamu wa Rare Earth na uendeshaji wa kina wa  mtambo wa majaribio  na upimaji, Peak Resources imepunguza kwa kiasi kikubwa sana hatari kutoka hatua ya uchimbaji mpaka katika mkondo wa usamabazaji wa bidhaa. Na rekodi inaonyesha kwamba timu ya Menejimenti inazo mbinu thabiti, za kufanikisha  na uelewa mzuri wa wateja na mahitaji yao. Timu ya utawala ina uelewano mzuri na tasnia na ina uwezo mzuriwa kujenga timu na kuzalisha bidhaa bora zenye mnyororo wa kuaminika na wa kudumu wa ugavi.

Graeme Scott

Afisa Mkuu wa Fedha
FCCA (UK)

Graeme ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika  kazi za kitaalamu na biasahara huko Australia na Uingereza. Alitumia miaka 12 iliyopita akifanyakazi katika sekta ya rasilimali katika majukumu ya Afisa Mkuu wa Fedha  majukumu ya kihaziri kwa makampuni yaliyoorodheshwa  ASX na TSX .

Rocky Smith

Ofisa Mtendaji Mkuu
BS Kemia, Biolojia, Fizikia

Rocky ana uzoefu wa  zaidi ya miaka 35 katika uendeshaji na  wa usimamizi mwandamizi katika sekta ya uchakataji madini & uhandisi wa kemikali na ameleta katika Kampuni ya Peak utaalamu wa kiutendaji, na uzoefu wa kiufundi katika uendeshaji Mradi wa  Rare Earth.

Michael Prassas

Meneja Mauzo ,Masoko,na Maenedeleo ya Biashara
Shahada ya Uchumi, Biashara za nje. Rasilimamli watu na Fedha

Michael ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika mauzo na masoko. Hasa katika mapatano ya mikataba ya muda mrefu ya usambazaji & mikataba ya uanzishwaji na akaunti za kimataifa kwa baadhi ya kampuni kubwa ya magari duniani na mkondo wa biashara za Rare earth.

Lucas Stanfield

Meneja Mkuu- Maendeleo
Shahada ya uhandisi wa Madini- MAUSIMM

Mhandisi wa uchimbaji wa madini mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika kazi za uchimbaji wa madini na uzoefu katika uongozi wa miradi katika Australia, Afrika na Uingereza. Uzoefu katika miundombinu na masuala ya kiufundi katika miradi huko Uingereza alipokuwa akifanya kazi kwa Global tier moja ya makampuni ya ujenzi na uhandisi.uzoefu katika kusimamia miradi mipya na upanuzi wa migodi na stadi za maendeleo